Maladie ya Ebola na maladie ya Marburg
Ebola na Marburg ni maladie za virus ambazo ni hatari sana na mara nyingi zinaweza kuua. Zinasababisha homa ya kuvuja damu. Virus hizi zinaenea kupitia contact ya moja kwa moja na damu au maji ya mwili ya mutu mwenye maambukizi. Maladie hizi mbili ziko na symptômes na namna ya kuenea karibu sawa. Ni test ya laboratoire tu inaweza kuonyesha tofauti kati ya hizo mbili.
Épidémies ya Ebola huko Congo na Uganda
Kwa sasa, kuna Épidémies ya Ebola katika République démocratique du Congo na Uganda.
Hatari ya maladie kuenea Ulaya na Norway ni ndogo sana. Hata kama mutu mwenye maladie angefika huko, autorités za santé ziko tayari vizuri, na hatari ya maladie kuenea ni ndogo.
Ebola na Marburg zinaenezwa namna gani
Virus ya Ebola na ya Marburg inapatikana kwa aina mbalimbali za wanyama wa porini katika nchi nyingi za Afrika. Mutu anaweza kupata maambukizi kutoka kwa mnyama.
Baada ya hapo, maladie inaweza kutoka kwa mutu moja kwenda kwa mwingine kupitia contact ya moja kwa moja na damu au maji mengine ya mwili ya mutu mgonjwa. Kwa hiyo, watu ambao wako karibu sana na wagonjwa ndio wako katika hatari kubwa ya kuambukizwa. Hasa watu wanaoishi na wagonjwa au wanaoshughulikia miili ya watu waliokufa wako katika hatari ya kuambukizwa.Pia, personnel ya santé wanaotibu wagonjwa bila kutumia mesures za kutosha za kuzuia maambukizi wako katika hatari ya kuambukizwa.
Unaweza kuambukiza watu wengine tu wakati uko na symptômes za maladie. Hii inamaanisha kwamba huwezi kuambukiza watu wengine wakati wa période ya incubation, yaani muda kati ya siku uliambukizwa na siku ulianza kuwa mgonjwa. Kadiri maladie inaendelea, hatari ya kuambukiza wengine inaongezeka. Hatari inakuwa kubwa zaidi wakati wa kipindi cha kuvuja damu.
Virus hizi hazienei kupitia hewa wala kupitia contact ya kawaida, kama kuwa katika chumba kimoja na mutu mgonjwa au kupita tu karibu na mutu mgonjwa barabarani. Pia, hakuna hatari ya kuambukizwa kupitia climatisation kama unasafiri kwenye ndege moja na mutu mgonjwa. Hata hivyo, services za santé zitafuatilia abiria waliokaa karibu sana na mutu mgonjwa kwenye ndege.
Période ya incubation
Muda kati ya kuambukizwa na kuanza kwa symptômes unaweza kuwa kutoka siku 2 mpaka siku 21. Kama haujapata symptômes yoyote ndani ya siku 21 baada ya kuwa na contact na mutu mgonjwa, maana yake haujaambukizwa.
Symptômes za maladie ya Ebola na Marburg
Symptômes za kwanza si maalum. Zinaweza kuwa
- homa
- baridi
- kutapika
- kuharisha
- maumivu ya kichwa
- maumivu ya misuli na viungo
- uchovu
- maumivu ya tumbo
Baada ya siku 5 mpaka 7, mutu anaweza kuanza kuvuja damu na viungo vya ndani vya mwili vinaweza kuacha kufanya kazi vizuri.
Taux ya watu wanaokufa inaweza kutofautiana sana kutoka mlipuko moja mpaka mwingine (20 mpaka 90%). Hii inategemea uwezo wa kupata soins de santé, kufanya test na kupata traitement.
Ebola na Marburg ziko na symptômes zinazofanana. Ni test ya laboratoire inahitajika ili kuthibitisha kama mutu ako na maladie. Kama bado haujawa mgonjwa, haiwezekane kujua kwa uhakika kama umeambukizwa.
Traitement
Hakuna traitement inayoweza kuondoa virus yenyewe. Traitement inasaidia kumpa mgonjwa soins bora zinazowezekana na kupunguza symptômes.
Prévention
Kuna vaccin ya Ebola, lakini kwa sasa inatumiwa zaidi wakati wa milipuko ya maladie. Kazi inaendelea kutengeneza vaccin zingine, hasa vaccin ya Marburg.
Kwa watu wanaokaa katika nchi ambazo ziko na milipuko ya Ebola au Marburg, lakini hawajakuwa na contact ya moja kwa moja na watu wagonjwa, hatari ya kuambukizwa ni ndogo sana
Unaweza kujikinga na maladie hizi kwa
- kuepuka contact na watu wagonjwa au watu waliokufa
- kuepuka kuwa karibu sana na wanyama walio hai au waliokufa, hasa singe, panya na chauves-souris
- kutokwenda kwenye mapango na sehemu zingine ambako chauves-souris wanaishi
- kutokula wala kutayarisha nyama ya porini, yaani nyama ya wanyama wa porini
Maswali na majibu kuhusu maladie ya Ebola na Marburg
Ufanye nini baada ya kurudi kutoka nchi yenye mlipuko?
Kama hukuwa na contact na mutu mwenye Ebola au Marburg
Kama uko na afya nzuri, hauna symptômes za maladie na hukuwa na contact na mutu mwenye Ebola au Marburg, huhitaji kuchukua précautions maalum.
Kama unapata homa au symptômes zingine baada ya kurudi kutoka sehemu yenye mlipuko, unapaswa kuwasiliana na médecin, hata kama hukuwa na contact ya moja kwa moja na mutu mwenye Ebola au Marburg. Inaweza pia kuwa muhimu kuangalia kama hauna maladie zingine, kama malaria. Mwambie médecin kwamba ulikuwa katika sehemu yenye mlipuko, ili aweze kukuuliza maelezo zaidi kama inahitajika.
Kama ulikuwa na contact na mutu mwenye Ebola au Marburg
Kama ulikuwa katika sehemu yenye mlipuko na ulikuwa na contact ya moja kwa moja na mutu mgonjwa au aliyekufa kwa Ebola au Marburg, piga simu kwa médecin na umwambie kwamba ulikuwa contact ya mgonjwa. Hii inatumika hata kama uko na symptômes au hauna symptômes.
Unapaswa kuangalia kama symptômes zozote zinatokea ndani ya siku 21 baada ya contact na mutu aliyeambukizwa.
Kama una homa ya zaidi ya 38 °C, iwe iko pamoja na kichefuchefu, kutapika, kuharisha au kuvuja damu bila sababu inayojulikana:
- Jitenge nyumbani
- Piga simu kwa médecin mara moja
- Mwambie kwamba ulikuwa katika sehemu yenye mlipuko na kwamba ulikuwa contact ya karibu na mgonjwa
Nitaonana na mutu anayeishi katika nchi yenye mlipuko. Ninapaswa kuchukua précautions maalum?
Kama mutu huyo ako na afya nzuri na hana symptômes za maladie, huhitaji kuchukua précautions maalum. Hakuna sababu ya kuzuia kukutana na watu wanaotoka katika sehemu zenye mlipuko.
Norway iko na mpango gani wa urgence kama mutu anapatikana na Ebola au Marburg nchini?
Kama mutu anapatikana na maambukizi ya Ebola au Marburg nchini ya Norvège, atawekwa peke yake katika service spécialisé. Hatari ya maladie kuenea ndani ya nchi ni ndogo sana. Norvège iko tayari vizuri kukabiliana na hali kama hii.
Kwa habari zaidi kuhusu Ebola na Marburg, unaweza kuangalia site ya Institut norvégien de santé publique
Contenu ilitolewa na qualité ili hakikishiwa na Folkehelseinstituttet
Kutiya bupia ya mara mwisho